TIMU YA CHELSEA IMEFUFUA AZMA YA KUMSAJILI VICTOR OSIMHEN KUTOKA GALATASARAY

Chelsea imefufua azma ya kumsajili Victor Osimhen kutoka Galatasaray baada ya kuanzisha makubaliano na timu ya Napoli kabla ya Januari.
Victor Osimhen alikuwa Napoli kabla ya kuenda Galatasaray kwa mkopo.
Osimhen, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Nigeria, alikuwa miongoni mwa walengwa wakuu wa Chelsea.
Napoli walikuwa tayari kumwachilia aende msimu wa joto baada ya kumsajili Romelu Lukaku kutoka Chelsea kama mbadala wake.
Awali, kwenye dirisha la uhamisho, Osimhen hakuwa na nia ya kujiunga na timu yoyote ya ligi ya Saudi Arabia ingawaje Al- Ahli ilikuwa inammezea mate na baadaye kumsajili Ivan Toney kutoka Brentford kama mbadala wake kwa bei nafuu.
Osimhen amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa vya Uropa katika miaka za hivi karibuni. Kwa sasa timu ya Galatasaray haina nia ya kuwa na mchezaji huyo kwa muda mrefu.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro