#Local News

MAREKANI KUIPA KENYA NDEGE 16, MAGARI 150 YA KIUSALAMA- WHITEHOUSE

Ikulu ya Whitehouse nchini Marekani imetangaza kwamba serikali hiyo imeipa Kenya ndege 16 aina za helikopta ili kuimarisha juhudi za Kenya kudumisha amani ndani na nje ya mipaka yake, kutokana na ziara ya Rais William Ruto nchini humo.

Ndege hizo zikiwemo nane za Hueys na nane aina ya MD-500 pamoja na magari 150 ya kiusalama, zinatarajiwa kuwasili humu nchini kati ya mwishoni mwa mwaka hu una mapema mwaka ujao.

Awali akizungumza baada ya kumpokea Rais William Ruto, rais wa Marekani Joe Bidden ametangaza kuendelea kushirikiana na Kenya kuimarisha demokrasia na sekta ya teknolojia na uvumbuzi.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *