#Local News

WATALII 5 WAFA KWENYE AJALI NYANDARUA

Watalii 5 wenye asili ya Kihindi wamethibitishwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kwenye ajali ya baada ya basi dogo walimokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Gichaka, kwenye barabara ya Nakuru kuelekea Ol-Joro Ork kaunti ya Nyandarua.

Imearifiwa kuwa watalii hao walikuwa wakisafiri kutoka mbuga ya Wanyama ya Maasai Mara kabla ya breki za basi hilo kufeli kwenye mteremko na kubingiria mara kadhaa.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Nyandarua Stella Cherono, 5 hao walifariki papo hapo ila mansura wakapelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya kaunti hiyo kwa matibabu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *