#Local News

MASHIRIKA 47 YAVUNJWA

Kama njia mojawapo ya kubana matumizi ya fedha za umma baadaa ya kutupiliwa mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024, Rais William ruto ametangaza mikakati ambayo imechukuliwa na serikali, ikiwemo kuvunja mashirika 47 ambayo huendesha shughuli zinazofanana.

Katika hotuba kwa taifa, Ruto amesema mashirika hayo hayajakuwa yakitengeneza faida, huku yakitumia mabilioni ya fedha za mlipa ushuru.

Aidha, Rais amesema majukumu ya mashirika husika na wafanyakazi wake watahamishiwa kwenye wizara mbali mbali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MASHIRIKA 47 YAVUNJWA

CAS, WASHAURI WACHONGWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *