#Local News

MAHAKAMA YAWAPA WANAUME AFUENI

Ni afueni kwa wanaume kufuatia uamuzi wa mahakama kuu ambao umetangaza kuwa kinyume na katiba kipengee cha 29 cha sheria za urithi, ikisema kipengee hicho kinawabagua wanaume waliofiwa na wake zao.

Kwenye uamuzi wake, jaji Lawrence Mugambi ameauru kuwa kipengee hicho kinachowataka wanaume kuthibitisha kuwa walikuwa wakiwategemea wake zao kimaisha kabla ya kupewa sehemu ya urithi wa mke anapofariki, kinakiuka katiba kuhusu usawa na kutobagua.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na mwanamme aliyetambuliwa kama mume wa marehemu Caroline Wawira, aliyedai kunyimwa sehemu ya urithi wa mkewe licha ya kutengana kabla ya kifo cha Wawira.

Imetayrishwa na Antony Nyonesa

MAHAKAMA YAWAPA WANAUME AFUENI

AFUENI KWA KYLIAN MBAPPE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *