KINDIKI AENDELEZA KAMPENI ZA MICHANGO
Naibu rais Kithure Kindiki ameendeleza kampeni zake na kuchangisha fedha kwa makundi ya akina mama, akidai anawapa uwezo wa kifedha.
Kindiki ameratibiwa kuzuru kaunti ya Kilifi hii leo, baada ya mikutano sawa katika kaunti ya Taita Taveta hapo alikokuwa ameandamana na viongozi mbali mbali akiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula.
Wameendelea kuwashutumu viongozi wa upinzani kwa madai ya ukabila.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































