DAVJI ATELLAH; AKAUNTI YA KMPDU YA X IMEDUKULIWA

Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari, nchini (KMPDU) Davji Atellah amesema kwamba akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa X imedukuliwa.
Katika taarifa ya leo Jumatatu, Atellah amekanusha kusimamishwa kwa maandamano yao yaliyopangwa “Occupy MOH”.
Ameongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kurejesha udhibiti wa akaunti hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete