#Local News

SERIKALI KUHAKIKI SERA ZA KIGENI

Katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei amesema serikali imeanza kutathmini sera za kigeni ambazo zimekuwa zikitumika tangu mwaka 2014 lengo likiwa kuwajumuisha wananchi katika utekelzaji wa sera hizo.

Aidha, Sing’oei amesema kuwa mapendekezo hayo ya sheria yatajumuihswa mwanzo katika mchakato wa kuwashirikisha wananchi ili kukusanya maoni ya washikadau kabla ya kuwasilishwa kwa baraza la mawaziri na kisha bungeni.

Sera hizo ambazo zinatoa mfumo wa namna Kenya inahusiana na mataifa ya kigeni, zimejikita kwenye mihimili mitano ya diplomasia.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *