#Local News

WAKENYA WAFELI KUJISAJILI KWA SHIF, SERIKALI YASEMA

Imebainika kwamba ni wakenya takribani 464,000 pekee ndio wamejisajili kwenye mpango wa afya ya jamii yaani SHIF inayolenga kuhakikisha afya kwa wote tangu uzinduzi wa usajili huo mnamo tarehe 1 mwezi huu, serikali ikitaja kesi za kupinga mpango huo kuwa miongoni mwa vizingiti.

Kupitia taarifa, katibu katika idara ya huduma za kimatibabu Harry Kimutai amesema lengo la serikali lilikuwa ni kuwasajili wakenya milioni 15 kwenye mpango huo katika kipindi cha siku 30.

Aidha, Kimutai ametaja ukosefu wa huduma za kimtandao kwa baadhi ya wakenya kuwa kizingiti zaidi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKENYA WAFELI KUJISAJILI KWA SHIF, SERIKALI YASEMA

KUWA MWALIMU NI MWITO

WAKENYA WAFELI KUJISAJILI KWA SHIF, SERIKALI YASEMA

POLISI WAMHUSISHA GACHAGUA NA MAANDAMANO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *