VISA VYA UHALIFU VYAPUNGUA MALINDI

Idara ya usalama katika kaunti ya Kilifi imedhibitisha kupungua kwa visa vya utovu wa usalama hasa katika wadi ya gada.
Kwa mujibu wa Judith mulei ambaye ni msaidizi wa naibu kamishina eneo la Malindi hatua hiyo imetokana na juhudi za idara hiyo za kukabili uhalifu na kuwahamasisha vijana kuhusu umuhimu wa kudumisha amani.
Mulei vile vile amewataka viongozi wa vijana kushirikiana na idara za usalama ili kuwahamasisha vijana zaidi umuhimu wa kudumisha amani na utulivu na vile vile kujiepusha na visa vya utulivu na kwamba idara ya usalama itawakabili kisheria watakaojihusisha na uhalifu.
Imetayarishwa na Janice Marete