WAKULIMA WA MIWA BUSIA WALALAMIKIA SIASA DUNI

Wakulima wa miwa katika kaunti ya Busia wamewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuhujumu utendakazi wa kiwanda cha sukari cha Mumias kwa lengo la kuzipa kampuni nyingine za sukari katika kaunti hiyo fursa ya kuendelea kuwahujumu.
Wakiongozwa na Mary Amoit, John Omachar na Peter Nyongesa, wakulima hao wamedai kunyanyaswa na kampuni hizo huku miwa yao ikiendelea kukauka mashambani baada ya kukatwa.
Wamewataka viongozi wanaopinga kufufuliwa kwa Busia Outgrowers Company BOCO kukoma, huku wakiipongeza hatua ya Mumias kununua miwa yao kwa bei wanayosema ni nzuri, mbali na kukubali kuzikarabati trekta za BOCO.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa