#Athletics #Sports

SIFAN HASSAN ADHIBITISHA UWEPO WAKE

Nyota wa mbio ndefu wa Uholanzi Sifan Hassan alitangaza Jumatano kuwa atakimbia marathon pamoja na kutetea taji lake la Olimpiki katika mbio za mita 5,000 na 10,000 alizoshinda Tokyo, huku akisaka mataji matatu ya kihistoria.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anatafuta kuwa mwanamke wa kwanza kushinda dhahabu katika mashindano hayo matatu, akimuiga mwanariadha mashuhuri wa Czech Emil Zapotek, ambaye alishinda mara tatu kwa wanaume huko Helsinki mnamo 1952.

Hassan si mgeni katika kuweka historia. Katika Michezo ya Tokyo, alikuwa mwanariadha wa kwanza kuwahi kushinda medali (mbili za dhahabu, moja ya shaba) katika mbio za 1,500m, 5,000m, na 10,000m.

Kuacha mbio za mita 1,500 ili kukimbia marathon ni hatua isiyotabiriki matokeo yake, alikiri, ingawa si mgeni wa mafanikio ya mbio hizo kwani alishinda mbio za London Marathon mwaka jana.

Fainali ya mita 10,000 imeratibiwa saa tatu usiku siku ya Ijumaa tarehe 9 Agosti, saa 35 pekee kabla ya mbio za marathon kuanza saa tatu asubuhi Jumapili ya tarehe 11 Agosti.

Kabla ya hapo, atakimbia mbio za mita 5,000 siku ya Ijumaa na kuna uwezekano wa fainali kuandaliwa Jumatatu jumla ya kilomita 62.195 za mashindano ya Olimpiki.

Imetayarishwa na Nelson Andati

SIFAN HASSAN ADHIBITISHA UWEPO WAKE

MATANO APASUA MBARIKA

SIFAN HASSAN ADHIBITISHA UWEPO WAKE

MBAPPE AMILIKI LIGUE 2

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *