#Local News

MCHAMBUZI WA MITANDAO YA KIJAMII GABRIEL OGUDA AACHILIWA

Mchambuzi maarufu wa mitandao ya kijamii Gabriel Oguda ameachiliwa baada ya kuripotiwa kutekwa nyara na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi.

Kuachiliwa kwake kumethibitishwa na mtumiaji wa X Nyandia Gachago Jumatano ambaye amesema Oguda Yuko salama” baada ya kushiriki picha inayoonyesha watu wanne kati yao Oguda ambaye alitoweka tangu siku ya Jumanne asubuhi.

Kukamatwa kwake kumehusishwa na msimamo wake mkali mtandaoni dhidi ya Mswada wa Fedha wa 2024 ambao umezua maandamano kote nchini.

Ripoti za kutekwa nyara kwake zilishirikiwa pamoja na wasiwasi kwamba watu wengine nyuma ya kurasa za X Franje, Drey Mwangi na Osama Otero, pia walitekwa usiku kucha jambo ambalo lilizua taharuki kwa umma.

Imetayarishwa na Janice Marete

MCHAMBUZI WA MITANDAO YA KIJAMII GABRIEL OGUDA AACHILIWA

KWA NINI RUTO ASIIDHINISHE MSWADA WA FEDHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *