ODINGA ASHINIKIZA FIDIA KWA WAATHIRIWA GEN Z

Kinara wa ODM Raila Odinga amejiunga na kauli za viongozi wa upinzani kumshinikiza Rais William Ruto kuwafidia waathiriwa wa maandamano ya yaliyoongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z mwaka jana, akisema hiyo ndiyo njia pekee ya kuliwezesha taifa kusahau madhila yaliyotokea na kusonga mbele.
Akizungumza wakati sherehe za Madaraka kwenye kaunti ya Homa Bay, Odinga aidha amemtaka Rais kulinda ugatuzi nchini na kuhakikisha kuwa serikali kuu haiingilii mamlaka ya kaunti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa