#uncategorized

MISHENI YA HAITI YAPATA PIGO, TENA

Mpango wa kenya kuwatuma maafisa wa polisi nchini Haiti umepata pigo kwa mara nyingine, baada ya wakili Ekuru Aukot kuelekea mahakamani akitaka mahakama kusimamisha mpango huo, akisema serikali imekiuka agizo la mahakama la Jaunuari kusitisha mpango huo.

Katika ombi lake, anasema serikali tayari imewachagua maafisa 200 wa polisi ambao wameratibiwa kuondoka mwishoni mwa wiki hii.

Aidha, amesema serikali inakiuka sheria maksudi kwa kuendelea na alichokitaja kuwa ni shughuli haramu ya kuwatuma polisi Haiti.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *