#Local News

WAZIRI WA ZAMANI BETT, WENGINE WATATU WAJERUHIWA KATIKA AJALI BARABARA YA AWASI-KERICHO

Waziri wa zamani Franklin Bett alikimbizwa hospitalini Jana Alhamisi baada ya kujeruhiwa katika ajali kwenye barabara ya Awasi-Kericho, Kaunti ya Kisumu.

Abiria wengine wawili waliokuwa kwenye gari lake na dereva wake pia wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali,

Polisi wanasema kisa hicho kilitokea mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia leo katika eneo la Karange kando ya barabara ya Awasi-Kericho.

Inaaminika kuwa dereva wa Bett hakuona trekta lilikuwa mbele yake kwani halikuwa na alama yoyote.

Trekta halikusimama baada ya ajali hiyo huku dereva akielekea kusikojulikana.

Imetayarishwa na Janice Marete

WAZIRI WA ZAMANI BETT, WENGINE WATATU WAJERUHIWA KATIKA AJALI BARABARA YA AWASI-KERICHO

TOTTE YAMSIMAMISHA BISSOUMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *