MAANDAMANO YA USHURU MOMBASA
Licha ya serikali kuondoa baadhi ya vipengee kwenye mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25, wakazi katika kaunti ya Mombasa wanaendeleza maandamano dhidi ya mswada huo, wanaosema unamkandamiza mwananchi.
Wakiwa na mabango, wakazi hao wamendamana katikati mwa jiji la Mombasa wakilenga kuwashinikiza wabunge wao kutupilia mbali mswada huo.
Aidha, wakazi hao wamedai kuwa hatua ya kuondoa baadhi ya vipengee kwenye mswada huo inalenga kuwafumba macho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































