MACHOGU AWAPA HABARI NJEMA WAZAZI, WANAFUNZI
Waziri wa elimu Ezekiel Machogu ametangaza kwamba zoezi la kutuma maombi kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa KCSE mwaka jana kupokea mikopo na ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu na kiufundi litaanza rasmi hapo kesho kupitia njia ya mtandao.
Katika taarifa, Machogu amesema zoezi hilo lilifaa kuanza Jumamosi iliyopita ila likasongeshwa hadi hapo kesho Jumanne kutokana na agizo la serikali kutangaza siku ya leo kuwa siku kuu.
Aidha, Machogu amewahakikishia wazazi na wanafunzi muda wa kutosha kutuma maombi hayo kabla ya tovuti kufungwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































