UCHUNGUZI BAADA YA MOTO KUTEKETEZA DUKA LA BUNGE LA KAUNTI YA MIGORI

Polisi katika Kaunti ya Migori wanachunguza hali ambapo moto umeteketeza duka la bunge la kaunti
Kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Suna Mashariki Ezekiel Kiche amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mfanyakazi wa bunge la kaunti alikuwa akichoma taka katika eneo la kuzoa taka moto huo uliposambaa hadi kwenye chumba cha kuhifathi chakula
Kiche amesema duka hilo la muda liliteketezwa na moto kabla ya mashine ya kuzima moto ya kaunti hiyo kuizima.
Imetayrishwa na Janice Marete