KUNA MANUFAA MENGI YA KIUCHUMI KUFUATIA MAGUEZI YA AU, RAIS RUTO

Bara la afrika kwa jumla limepata fursa za kipekee za biashara wiki hii baada ya umoja wa afrika kufanya mageuzi makubwa ya kitaasisi, mageuzi ambayo yanaashiria enzi mpya ya muungano wa kiuchumi kwa bara la afrika.
Rais wiliam Ruto ambaye walihutubu wakati wa ufunguzi wa Shirikisho la Wafanyabiashara Duniani uliofanyika jijini Nairobi, amesema kuwa ni fursa ya kukumbatiwa na bara la Afrika kwani kuna manufaa mengi.
Ruto aidha amesema kuunda upya mashirika mengi muhimu yakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Uuzaji na Uagizaji Bidhaa ya Afrika, Taasisi ya Mendeleo ya Umoja wa Afrika pamoja na taasisi nyingi za kiuchumi za kikanda, kunaleta matumaini kwa Afrika, na kuweka msingi wa ustawi unaohimizwa na uwekezaji, ukuaji wa viwanda, utengenezaji bidhaa kwa ajili ya masoko ya kimataifa, na biashara.
Vile vile, amesema matokeo ya mageuzi hayo ni kuwa kampuni za utengenezaji na kampuni changa za teknolojia za Kenya zinaenea barani kote, na kuonyesha imani kwamba mustakbali wa kiuchumi wa Afrika uko katika biashara na ushirikiano kati ya nchi za bara hili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa