IDARA YA MAHAKAMA BUNGOMA YAZINDUA COURT ANNEXED MEDIATION

Idara ya mahakama kaunti ya Homa Bay imezindua mpango wa kuwaruhusu watu walio na kesi mahakami kusuluhisha kesi hizo nje ya mahakama mpango wanauita Court Annex Mediation kama hatua ya kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani.
Jaji wa mahakama ya homa bay Kiarie Waweru, hakimu mkuu wa mahaka hiyo Jesinta Orwa na mwenyekiti wa chama cha sheria LSK wa kaunti hiyo Nancy Nyarige wameongoza hafla ya kuzindua mpango huo.
Jaji Kiarie anasema wamechukua hatua hiyo kutokana na kesi zilizowasilishwa mahakamani ambazo zinaweza kutatuliwa nje ya mahakama.
Kwa upande wake hakimu Jesinta Orwa mbinu hiyo ina manufaa mengi ikiwemo kuboreesha uhusiano baina ya watu waliokosana katika jamiiNaye mwenyekiti wa chama cha wanasheria kaunti ya homa bay Nancy nyarige amesema LSK inaunga mkono kikamilifu mpango huo.
Imetayarishwa na: Janice Marete.