MGOMO: WAKAZI WA KISII WAPATA AFUENI
Ni afueni kwa wakazi wa kaunti ya Kisii baada ya mgomo wa wahudumu wa afya uliokuwa umeratibiwa kuanza hii leo kuahirishwa.
Hatua hiyo imejiri baada ya serikali ya kaunti hiyo kuelewana na uongozi wa miungano ya wahudumu hao kuhusu malalamishi yao.
Akizungumza katika hospitali ya rufaa mjini Kisii, Waziri wa afya Ronald Nyakweba ameahidi kwamba wahudumu waote wataongezwa mishahara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































