SARAH MORAA ATARAJIA KUBEBA TAJI.

Bingwa wa Afrika wa mbio za mita 800 Sarah Moraa anajiandaa kubeba taji lake la kwanza la kimataifa katika Mashindano ya Dunia ya Vijana walio chini ya umri wa miaka 20 yaliyopangwa kufanyika Agosti 27-31 mjini Lima, Peru.
Ingawa hakufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris iliyomalizika majuzi, Sarah anasema hakuna kilichopotea huku nguvu zote zikielekezwa kwa Ubingwa wa Lima.
Sarah anashukuru kwa kambi za riadha za likizo ya shule zinazoandaliwa na shirikisho la riadha nchini AK, akisema zimemuimarisha zaidi katika mbio hizo za mizunguko miwili.
Imetayarishwa na Nelson Andati