#Local News

ASKARI MAGEREZA AFARIKI KWA KUJITOA UHAI BAADA YA KUMUUA MKEWE HUKO KITUI

Polisi wameanzisha uchunguzi bada ya Askari magereza kudaiwa kujitoa uhai baada ya kumuua mkewe katika kisa cha kushangaza kilichotokea katika kaunti ndogo ya Mwingi Magharibi kaunti ya Kitui.

Askari huyo ambaye alikuwa amefungwa katika Gereza la Garissa GK akiwa amejihami kwa panga alikabiliana na mkewe, mwalimu wa shule ya msingi, na kumkatakata hadi kufa baada ya ugomvi.

Kisa hicho kimethibitishwa na kamanda wa polisi wa eneo hilo Ephantus Kenyatta abaye amesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 54 alimtuhumu mkewe mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi ya Kateiko kwa kosa la kukosa uaminifu.

Ameongeza kuwa mtoto wa wanandoa hao ambaye alikuwa amekwenda kuwatembelea wazazi wake katika nyumba yao alikuta mwili wa mama yao ukiwa kwenye dimbwi la damu chumbani na kutoa taarifa polisi.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *