MATAIFA YA AFRIKA MASHARIKI WASHIRIKI MCHUJO WA AFCON

Kenya, Uganda na Tanzania zitacheza mchujo wa kuwania kufuzu Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) 2025 licha ya mataifa hayo matatu kuwa waandaji wenza wa michuano hiyo na wakiwa tayari wamehakikishiwa tiketi ya kushiriki.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mataifa hayo matatu yatacheza mechi za kufuzu kwa ukanda wa CECAFA, lakini ikiwa ni jukwaa la kujiandaa na michuano hiyo, huku ukanda huo ukiwa na uhakika wa timu nne, kwani moja zaidi itaungana na wenyeji.
Raundi ya kwanza ya mchujo huo imepangwa kufanyika Oktoba 25-27 na Novemba 1-13 mwaka huu huku awamu ya pili ikichezwa Desemba 20-22 na Desemba 27.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika Februari 1-28. Kenya itakuwa mwenyeji wa michezo hiyo katika viwanja vya Moi Sports Centre Kasarani na Nyayo Stadia.
Imetayarishwa na Nelson Andati