#Local News

POLISI AFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA POLISI MJINI BUNGOMA

Afisa wa polisi katika Kaunti ya Bungoma ameaga dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari la polisi alipokuwa akitekeleza majukumu yake katika eneo la Cheptais Junction.

Fredrick Juma aliyejiunga na Kitengo cha Ulinzi wa Miundombinu (CIPU) huko Bungoma Magharibi amekumbana na mauti aliposimamisha trela kwa ukaguzi wa kawaida alipokuwa akimuhoji dereva huyo, aliangushwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser la Kituo cha Polisi cha Sirisia lililokuwa likielekea upande mwingine.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *