MASOMO YATATIZIKA CHUONI MOI KUSU IKIJIUNGA NA UASU
Shughuli za masomo katika chuo kikuu cha Moi zimesambaratika hata zaidi baada ya muungano wa wafanyakazi wa vyuo vikuu KUSU eneo hilo kujiunga na wenzao wa UASU kwenye mgomo ambao umelemaza masomo kwa wiki ya tatu sasa.
Wanachama wa UASU na KUSU wameandamana jijini Eldoret wakishinikiza kulipwa mishahara yao na kuwasilisha matozo ya fedha za uzeeni ambazo ni zaidi ya bilioni 5 kwa bodi husika.
Katibu mkuu wa KUSU tawi la Moi Mary Chepkwemoi amekitaka chuo hicho kutekeleza makubaliano yaote, naye mwenzake wa UASU Nyabuta Ojuki akiulaumu usimamizi wa chuo hicho kwa madai ya kukosa kushirikiana na wizara ya leba kumaliza mgomo huo.
Haya yanajiri huku naibu mwenyekiti wa UASU Cyprian Ombati akisisitiza kwamba mgomo utaanza kwenye vyuo vyote nchini ndani ya siku 7 zijazo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































