BANDARI WAKO TAYARI KUMENYANA NA GOR

Timu ya Bandari fc imeweka wazi kwamba wako tayari kupambana na Gor Mahia hapo kesho katika mechi ya ligi kuu nchini KPL.
Mechi hiyo inatarajiwa kuandaliwa katika uwanja wa maonyesho ya kilimo wa Ukunda kaunti ya Kwale.
Kulingana na mkurungezi mkuu wa timu ya Bandari fc Tony Kibwana anasema haitakuwa mara ya kwanza kwa Bandari fc kutandika Gor hivyo hawana wasiwasi wa kuingia kwa mechi hiyo.
CEO Kibwana anasema timu hiyo imekuwa na matayarisho mazuri ya mechi hii licha ya kocha mkuu Ken Odhiambo, kocha wa makipa Jeremy Onyango na wachezaji watatu Siraj Mohammed, Fidel Origa na Bryne Omondi kuwa katika kikosi cha taifa wakati wa mechi ya marudiano ya kufuzu kwa CHAN dhidi ya Sudan Kusini.
Kufikia sasa Bandari fc hawajapoteza mechi yoyote msimu huu, wakipata ushindi mara 2 na kukabwa sare mara 3.
Imetayarishwa na Nelson Andati