MIGUNA” MATIANG’I HAFAI KUWA RAIS”
Azma ya aliyekuwa waziri wa usalama Fred Matiang’i kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao imeendelea kuibua hisia mseto, wakili mwenye utata Dakta Miguna Miguna akishikilia kuwa Matiang’i hafai kuliongoza taifa hili kutokana na ukiukaji wa amri za mahakama alipokuwa waziri.
Kwenye mahojiano na runinga moja nchini, Miguna ametaja kufurushwa kwake nchini kwa lazima na uharibifu wa makazi yake, akikariri kuwa alitendewa ukiukaji huo chini ya amri ya waziri huyo wa zamani.
Kulingana naye, taifa halitapata mageuzi ikiwa Matiang’i atachaguliwa kuwa rais.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































