#Local News

FARMERS PARTY YAPANGA MAANDAMANO KUMREJESHA GACHAGUA

Chama cha Farmers kimesema kitafanya maandamano kuelekea makazi rasmi ya Naibu Rais, Rigathi Gachagua, huko Karen, Nairobi, baada ya Mahakama ya Rufaa kufutilia mbali uamuzi wa Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu wa kuunda jopo la majaji kusikiliza ombi la kumng’atua Gachagua.

Gachagua aliondolewa serikalini Oktoba 18 kupitia pendekezo la Seneti, na Kindiki aliteuliwa kama mrithi wake.

Timu ya kisheria ya Gachagua ilipinga uamuzi huo, ikisema ni Jaji Mkuu pekee anayeweza kufanya uteuzi huo huku Mahakama ya Rufaa ikielekeza suala hilo lipelekwe kwa Jaji Mkuu. Gachagua ameahidi kupata haki kutoka kwa mahakama.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *