UCHUNGUZI WA FIGO WATUA ELDORET
Serikali inaendeleza juhudi za kutegua kitendawili cha upandikizaji wa viungo vya mwili ikiwemo figo na madai ya ulanguzi wa viungo hivyo katika hospitali ya kibinafsi ya Mediheal, tayari malalamishi ya wananchi yakianza kupokelewa jijini Eldoret.
Mwenyekiti wa kamati inayochunguza huduma za upandikizaji huo profesa Elizabeth Bukusi, amewataka wakazi walio na malalamishi kuhusu huduma hizo katika vituo mbali mbali vya afya kutoa maoni yao ili kufanikisha uchunguzi unaoendelea.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































