UMMA WAJERUHI POLISI NYAMIRA

Maafisa wa polisi katika eneo la Kimera kaunti ya Nyamira wamelazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanya wakazi waliowashambulia kwa mawe na kuwajeruhi maafisa wawili.
Imeripotiwa kuwa maafisa wa polisi walikuwa wamefika katika eneo hilo kuwmokoa mwanamme aliyekuwa akishambuliwa na umma baada ya kudaiwa kuhusika katika mauaji.
Aidha, kioo cha gari la polisi aina ya landcruiser kimeharibiwa, huku mali ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 ikiharibiwa.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa