#uncategorized

WAITITU ASEMA MASHTAKA YA UFISADI YA KSH.588M YANACHOCHEWA KISIASA.

Kesi ya ufisadi wa shilingi milioni 588 dhidi dhidi ya alikyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, mkewe Susan Wangari na washukiwa wengine itaendelea leo hii.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 32 katika kesi hiyo, jaji ya mahakama ya ufisadi Thomas Nziuki aliwapata washukiwa hao na kesi ya kujibu  baada ya kupekua stakabadhi za kesi dhidi yao.

Waititu na washukiwa wenza wanatarajiwa kujitetea dhidi ya madai hayo katika vikao ambavyo vinatarajiwa kuendelea leo hii.

Jumatano waititu aliyakana mashtaka hayo na kuiomba mahaka kumwondolea kesi hiyo.

Kwa mujibu wa waititu mashtaka hayo yanamwandama baada ya kuanza kushirikiana na rais William Ruto wakati huo akiwa naibu wa rais mwaka 2022.

Imetayarishwa na: Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *