‘DISHI NA KAUNTI ITAENDELEA ‘ SAKAJA ASEMA

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amewahakikishia wazazi na wanafunzi kwamba mpango wa kulisha shuleni wa Dishi na County katika kaunti ya nairobi hautaathiriwa na mpango wa serikali ya kitaifa wa kukomesha programu za kulisha shuleni.
Haya yanajiri baada ya Hazina ya Kitaifa kutoa pendekezo la kutupilia mbali mgao wa fedha wa mpango wa lishe shuleni katika makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2024/2025.
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































