IG KANJA AFICHUA MLALAMISHI KWENYE KIFO CHA ALBERT OJWANG
Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja amethibitisha kuwa mwanablogu Albert Ojwang’ aliyefariki katika kituo cha polisi cha Central Jijini Nairobi alikuwa akiechunguzwa kwa madai ya kumchafulia jina naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kwenye mitandao ya kijamii.
Katika taarifa kwa wanahabari, Kanja amesema naibu wake alikuwa amewasilisha malalamishi rasmi ya kuchafuliwa jina na mwnablogu huyo.
Hata hivyo, amesema tayari uchunguzi unaendelea ili kubaini kilichosababisha kifo hicho, ikiwemo kuwasimamisha kazi maafisa kadhaa wa kituo cha polisi cha Central.
Imetayarishwa na Maureen Amakhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































