KABRAS WAZIDI KULAMBA SUKARI

Kabras RFC ilishinda mkondo wa christie sevens wa msururu wa kitaifa wa 7s baada ya kuwalaza wenyeji kenya harlequins 17-12 katika fainali jana jumapili.
Akizungumza baada ya mechi ya fainali, kocha wa timu ya wachezaji saba wa kabras, felix khaemba alisifu azma ya timu yake kurejea katika njia za ushindi.
Kwa upande wake, kocha mkuu wa kenya harlequins paul murunga aliridhika na kumaliza kwa nafasi ya pili.
Katika mchujo wa nafasi ya tatu watawa wa kikatoliki ‘catholic monks’ walijinyanyua na kuwachabanga strathmore leos 10 -7 na kumaliza wa tatu.
Msururu huo sasa unaelekea kakamega kwa ingo sevens agosti 2-3.
Imetayarishwa na Janice Marete