#Sports

HUSTLER YADHIBITIWA

Bajeti ya Hazina ya Hustler Fund ilipunguziwa kiwango cha fedha katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/26 iliyosomwa na Waziri wa fedha John Mbadi tarehe 12 mwezi huu.

Hustler Fund imetengewa shilingi milioni 300, kutoka shilingi bilioni 5 iliyokuwa imetengewa katika mwaka wa fedha uliopita.

Hata hivyo, imebainika kuwa ni mara ya pili kwa hazina hiyo kupunguziwa mgao wa fedha kutoka kwa hazina ya fkitaifa licha ya hazina hiyo kuonekana kuwa kipaumbele kutoa mikopo nafuu kwa umma. Katika mwaka wa kifedha wa 2023/24, Hustler Fund, ambayo wakati huo ilikuwa fahari ya serikali ya Kenya Kwanza, ilitengewa shilingi bilioni 10 chini ya aliyekuwa Waziri wa fedha Njuguna Ndung’u.

Mgao wa Ksh.300 milioni na Mbadi ulikuwa chini sana kuliko matarajio ya wizara ya Maendeleo ya Biashara ndogo ndogo na za Kati, ambayo mwezi Mei iliwaomba wabunge kuidhinisha mgao wa shilingi bilioni 5 katika hazina hiyo katika mwaka wa kifedha wa 2025/26.

Imetayrishwa na Maureen Amwai

HUSTLER YADHIBITIWA

WAKENYA WATIA FORA DIAMOND LEAGUE

HUSTLER YADHIBITIWA

MARAGA: LAGAT AKAMATWE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *