NAKURU YATENGA MILIONI 100 ZA UKARABATI WA BARABARA

Kaunti ya Nakuru imetenga Shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu zilizoathiriwa na mvua iliyonyesha hivi majuzi na kusababisha uharibifu mkubwa
Pesa hizo zitatumika kutunza barabara muhimu katika kata zote 55, huku serikali ikitafuta bajeti ya juu zaidi kukarabati miundombinu hiyo.
Mvua kubwa ilinyesha nchini miezi mitatu iliyopita, na kuua makumi ya watu, kuharibu mali ya mamilioni na vile vile majengo.
Naivasha ilikuwa mojawapo ya maeneo bunge yaliyoathirika zaidi, baada ya bwawa la old kijabe kuvunja kingo zake na kupelekea vifo vya watu zaidi ya 60 huko Mai Mahiu na kuharibu barabara.
Imetayarishwa na Janice Marete