WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA CHUKA WAGOMA
Shughuli za biashara na usafiri zimetatizika katika barabara ya chuka meru kaunti ya Tharaka nyithi kufuatia maandamano yanayoendelea.
Maandamano hayo yanawahusisha wanafunzi wa chuo kikuu cha chuka wakilalamikia utovu wa usalama barabarani eneo la chuo hicho.
Wanafunzi hao wanahoji kuwa wenzao wamehusika katika ajali ya barabarani haswa katika eneo la Ndagani.
Wanaitaka serikali kupitia mamlaka ya barabara kuu nchini KENHA kuweka matuta kwenye barabara hiyo na vile ile kutenga sehemu ya wapiti njia kuvuka.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































