MAREKANI WALEMEWA KWA ROBO FAINALI
Timu ya taifa ya Marekani ilishindwa katika fainali ya Kombe la Dhahabu la CONCACAF kwa kuchapwa 2-1 na Mexico lakini itachukua mafunzo muhimu kutokana na michuano hiyo inapojizatiti kuelekea Kombe la Dunia mwaka ujao, kulingana na kocha Mauricio Pochettino.
Marekani walifungiwa na Chris Richards katika mchezo huo wa Houston, Texas lakini Mexico wakashinda kupitia Raul Jimenez na Edson Alvarez na kunyakua taji la 10 la Gold Cup.
Pochettino aliwaambia waandishi wa habari kwamba ingawa ulikuwa usiku wa maumivu kwa upande wake michuano hiyo ilikuwa ni maandalizi mazuri kwa Kombe la Dunia la 2026, ambalo Marekani itaandaa kwa pamoja na Mexico na Canada.
Marekani ilifika fainali licha ya kuwakosa wachezaji kadhaa muhimu, Christian Pulisic na Yunus Musah walijiondoa kwa utata huku Weston McKennie, Gio Reyna na Tim Weah hawakuweza kucheza kwa sababu ya majukumu ya Kombe la Dunia la Vilabu.
Walakini, Pochettino hakutaka kuzungumzia athari za kutokuwepo kwao.
Marekani itakaribisha Korea Kusini na Japan katika mechi za kirafiki mwezi Septemba.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































