#Local News

MWANAFUNZI WA MWAKA WA NNE WA CHUO KIKUU CHA PWANI AFARIKI HUKO KILIFI

Washukiwa wawili wamekamatwa kufuatia kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo kikuu cha Pwani huko Kilifi huku juhudi za kuwatafuta washukiwa zaidi zinzikiendelea.

Mwili wa mwanafunzi huyo umepatikana katika eneo la Kisumu Ndogo jana Jumapili muda mrefu baada ya kuuawa ukiwa na majeraha.

Haijabainika ni nini kilisababisha kifo cha mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 24.

Mwili huo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo ukisubiri uchunguzi.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *