STENCY NEEMA AWEKA HISTORIA KWA KENYA KATIKA OLIMPIKI YA WALEMAVU
Mchezaji wa taekwondo wa timu ya taifa ya Kenya, Stency Neema ameshindwa katika Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Paris kufuatia kulemewa 12-3 na mshindi wa medali ya fedha ya dunia ya 2023.
Salma Ali Abdi Al Moneem Hassan wa Misri katika hatua ya 16 bora kwa wachezaji walio chini ya kilo 52 kwa wanawake kitengo cha K44 katika ukumbi wa Grand Palais.
Licha ya kuondolewa kwake, Neema alikuwa Mkenya wa kwanza kushiriki taekwondo katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu na pia alikuwa Mkenya wa kwanza kushiriki katika Michezo ya Paris ya mwaka huu.
Mpinzani wake Hassan alimaliza wa saba kwenye Michezo ya Tokyo mnamo 2021 taekwondo ilipoanzishwa katika Michezo ya Walemavu.
Mwakilishi mwingine wa Kenya Julieta Moipo atachuana na Marija Mičev wa Serbia katika raundi ya 16 ya wanawake chini ya kilo 57 K44 kesho saa 11:56 asubuhi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































