#Local News

RUTO, COTU WAWAPA WAFANYAKAZI AFUENI

Wafanyikazi walio kwenye mshahara watapewa kipaumbele cha umiliki wa nyumba za bei nafuu kufuatia makubaliano kati ya Rais William Ruto na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli.

Wawili hao pamoja na wajumbe wao, walifanya mkutano wa faragha katika Ikulu hapo jana, uliolenga kukinga Hazina ya Ushuru wa Makazi dhidi ya kuelekezwa kwenye miradi tofauti.

Awali, Atwoli alikuwa amekosoa serikali kwa kukosa kushauriana na COTU kabla ya kuelekeza upya fedha za Ushuru wa Nyumba-zinazokatwa kwa lazima kutoka kwa mishahara ya Wakenya wanaolipwa- kuelekea ujenzi wa masoko 400 kote nchini.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

RUTO, COTU WAWAPA WAFANYAKAZI AFUENI

KIAMBU GOLFCLUB KUANDAA MAKALA YA 13 YA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *