GOR YAACHILIA WACHEZAJI WAKE

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amesema wazi kwamba watawaachilia wachezaji ambao kandarasi zao zimeisha, akifichua hawataongeza kandarasi zao.
Rachier aliongeza kuwa pia watawaachilia wachezaji walioshuka viwango, kuanzia na wenye kutotumika sana na wenye kukosa uthabiti.
Mwenyekiti huyo wa muda mrefu alisema hayo jana baada ya kutimua benchi zima la ufundi kufuatia matokeo mabaya ya msimu uliomalizika.
Mwenyekiti huyo wakati huo huo amewaondoa wasimamizi wote wa timu kusimamia lango uwnajani akisema kampuni ya tiketi italazimika kuweka wasimamizi wao wenyewe ili kuhakikisha hakuna pesa zinazoingia kwenye mifuko ya watu binafsi.
Hata hivyo anasema kila hatua itakuwa juu ya makubaliano ya pande zote ili kuepuka vikwazo vya FIFA.
Imetayarishwa na Nelson Andati