#Local News

GAVANA LENOLKULAL APINGA HUKUMU

Gavana wa zamani wa Samburu Moses Lenolkulal amekata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa na mahakama wiki jana baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi inayohusu shilingi milioni 83.4 alipokuwa mamlakani.

Kupitia kwa mawakili wake, Lenolkulal anasema kulikuwa na dosari katika hukumu hiyo na kumshutumu hakimu Thomas Nzioka kwa kukosa kufanya uchunguzi wa kina kwenye ushahidi, akiitaka mahakama kuifutilia mbali.

Kwenye uamuzi wa wiki jana, gavana huyo wa zamani alipewa kifungo cha miaka 8 gerezani au faini ya shilingi milioni 85.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GAVANA LENOLKULAL APINGA HUKUMU

GATUSSO AREJEA KIZIMBANI

GAVANA LENOLKULAL APINGA HUKUMU

TUKO PABAYA KIFEDHA, SRC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *