VIONGOZI AFRIKA WAMUUNGA ODINGA MKONO
Azma ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga kuwania wadhifa wa uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC imepigwa jeki baada ya viongozi mbali mbali wa bara la Afrika kutangaza kumuunga mkono.
Viongozi hao ni Pamoja na rais wa Uganda Yoweri Museveni, Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Salva Kiir wa South Sudan, rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo miongoni mwa wengine.
Wametangaza uamuzi wao katika ikulu ya Rais jijini Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































