#Business

RAIS RUTO AFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI NAIROBI

Uchumi wa taifa unaotokana na setka ya utalii unatarajiwa kuimarika kufuatia kufunguliwa kwa maonytesho ya kimataifa ya utalii jijini Nairobi na rais William Ruto ambaye amethibitisha dhamira yake ya kuongeza idadi ya watalii kutoka masoko yanayoibuka hadi milioni 5 kufikia mwaka wa 2027.

Maonyesho ya Utalii ya Magical Kenya 2024, ambayo ni maonyesho ya utalii yanayoongoza katika eneo la Afrika Mashariki na Kati, yatafanyika hadi Ijumaa, na yamevutia zaidi ya washiriki 4,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Maonyesho hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB), yanahudhuriwa na mawakala 180 wa usafiri wa kimataifa, wakiwemo 75 kutoka Afrika, 37 kutoka Amerika Kaskazini, 26 kutoka Ulaya, na 42 kutoka Asia na Mashariki ya Kati.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

RAIS RUTO AFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI NAIROBI

MOSES KURIA: KULIKUWA NA HAJA YA KUUNDA

RAIS RUTO AFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI NAIROBI

SHIRIKA LA RELI LA KENYA KRC LABORESHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *