#Sports

SIKUBALIANI NAO KATU!

Kocha mkuu wa klabu ya shule ya upili ya Ebwali Francis Muhambe amekashifu tangazo la serikali mwaka jana la kuwapandisha vyeo moja kwa moja walimu ambao timu zao zitashiriki katika mashindano ya kitaifa ya Chama cha Michezo cha Shule za Sekondari Kenya (KSSSA), kuwa sababu kuu ya udanganyifu katika michezo ya shule. .

Muhambe anasema hatua hiyo imeshuhudia shule kadhaa zikiwa tayari kuajiri njia zisizo za kawaida kuweka nafasi katika ngazi ya kitaifa.

Muhambe, ambaye alizungumza wakati wa mafunzo ya timu shuleni hapo, alisema kuna haja kwa uongozi wa KSSSA kuweka muhuri mamlaka yao ili kuepusha hatari ya kupoteza njama yake ya kufichua vipaji mbichi vya vijana.

Visa vya kuwachezesha wachezaji wasiostahili vilikithiri katika michezo ya shule hasa eneo la Nyanza, huku mwenyekiti wa KSSSA eneo la Nyanza Otieno Oloo akitoa onyo kuwa watakaopatikana na hatia watakabiliwa na mkono wa sheria.

Imetayarishwa na Nelson Andati

SIKUBALIANI NAO KATU!

MJOMBA AZIDI KUNAWIRI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *