#Local News

MWANAMKE AJICHOMA NA MWANAWE KASARANI

Maafisa wa polisi eneo la Kasarani jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo mwanamke kwa jina Ann Wanjala na mwanawe wameteketea hadi kufa ndani ya nyumba yao wakidaiwa kujiteketeza usiku wa kuamkia leo.

Imeripotiwa kwamba mwanamke huyo alikuwa na mumewe na wanawe mchana kutwa ndani ya nyumba yao kabla ya mumewe kuondoka jioni kuelekea kazini, kisha mwanamke huyo akamtuma mjakazi wake dukani na kisha kujifungia ndani ya nyumba na kuiwasha moto.

Majirani waliosikia mayowe walijaribu kuvunja mlango ila wakapata wawili hao wameteketea kiasi cha kutotambulika.

Miili yao inahifadhiwa katika makafani ya City.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWANAMKE AJICHOMA NA MWANAWE KASARANI

MSHTUKO MIILI 9 IKIPATIKANA MUKURU

MWANAMKE AJICHOMA NA MWANAWE KASARANI

SERIKALI YA HOMA BAY KUJENGA MADARASA 160

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *