WATU WAWILI WAFARIKI KWA KUJITOA MHANGA UASIN GISHU NA HOMA BAY

Maafisa wa upelelezi wanachunguza visa viwili tofauti vya kujitoa mhanga vilivyoripotiwa katika kaunti za Uasin Gishu na Homabay mtawalia.
Kisa cha kwanza ni cha Laban Kimeli ambaye mwili wake umepatikana katika nyumba yake katika kijiji cha Mogobich, Nandi, kisa ambacho kinashukiwa kuwa kujitoa mhanga.
Kwa mujibu wa Maafisa wa Polisi waliotembelea eneo la tukio, alijifunga kamba shingoni ili kujinyonga lakini akaanguka sakafuni baada ya kamba hiyo kukatika.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti ukisubiri uchunguzi
Kwingineko katika kijiji cha Kajie, Homabay, mwanamke mwenye umri wa miaka 60 anashukiwa kujiua kwa kujinyonga juu ya paa.
Hivi ndivyo visa vya hivi punde zaidi kuripotiwa katika hali inayotia wasiwasi nchini.
Imetayrishwa na Janice Marete